OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA NUSU MUHULA
015 ELIMU YA DINI YA KIISLAMU KIDATO CHA PILI
MUDA: SAA 2:30 MACHI
MAELEKEZO:
SEHEMU A (Alama 15)
Jibu maswali yote katika sehemu hii
1. Katika kipengele (i)-(x),chagua jibu sahihi kisha andika herufi yake katika kisanduku
(i) Wanataaluma wanatofautina mitazamo kuhusu chanzo sahihi cha elimu zote ulimwenguni.Ni upi mtazamo wa wanataaluma wa kiislamu ?
(ii) ‘Tuongoe njia iliyonyooka,sio ya waliokasirikiwa ,wala waliopotea’ (Suratul-faat-ha aya ya 7). Kwa mujibu wa tafsiri ya aya hii ni akina nani waliopotea?
(iii) Juma alisikia akiingiza herufi katika herufi nyingine na kuitamka kama moja wakati akisoma Qur’an.Je ni hukmu gani ya Taj-wiid iliyoanishwa na Juma?
(iv) Ni maneno aliyoyasema Mtume (S.A.W) au maelezo ya swahaba kuhusu alivyomuona Mtume(s.a.w) akitenda jambo.Hii ni maana ya istilahi gani kati hizi?
(v) Ni kwa muktadha gani dhana ya Hadith inafafanuliwa kama jambo au kitu kipya,taarifa au hotuba?
(vi) Umesujudu uso wangu kumsujudia Yule ambaye ameuumba na akajaalia usikivu wake na uoni wake kwa uwezo wa nguvu zake.Ametukuka Allah mbora wa waumbaji’.Hii ni dhikri inayoletwa wakati wa kuleta sijda gani?
(vii) Katika somo la fiqh kuna fiqh inayohusiana na mambo ya kisiasa,biashara na uchumi.Wafahamishe wanafunzi wenzio aina hii ya fiqh huitwaje?
(viii) Wanafunzi wa kidato cha pili wa mwaka huu 2026 wengi wao wamesahau nguzo za Da’awah baada tu ya kukaa likizo ya mwezi wa desemba.Je wewe kama kijana aliyejitahidi kusoma wakati wa likizo hiyo unakumbuka nguzo hizo? Wakumbushe wenzako.
(ix) Jambo gani katika maisha ya Nabii Adamu (A.S) linaonesha kuandaliwa kuwa Khalifa?
(x) Watu wa madian waliangamizwa kwa makosa mbalimbali waliyoyafanya isipokuwa
MAJIBU:
| i | ii | iii | iv | v | vi | vii | viii | ix | x |
| . |
2. Oanisha kila lengo lililopo Orodha A na Nguzo husika ya Uislamu iliyopo Orodha B kasha andika herufi ya jibu sahihi katika sehemu ya kuandikia majibu uliyopewa.
| Orodha A | Orodha B |
| (i) Kuthibitisha upweke wa Mwenyezi Mungu (s.w) na utume wa Mtume Muhammad (s.a.w), na kumuingiza mtu katika uislamu. (ii) Kumjenga Muislamu kiroho,kumuweka karibu na mwenyezi Mungu(s.w),na kumkinga na maovu (iii) Kutakasa mali na kusaidia wenye uhitaji ili kujenga mshikamano katika jamii (iv) Kumfundisha muislamu subira na kujidhibiti, pamoja na kukuza taqwa. (v) Kuimarisha umoja wa waislamu na kuimarisha utiifu kwa Mwenyezi Mungu. |
|
MAJIBU:
| i | ii | iii | iv | v |
| . |
SEHEMU B (Alama 70)
Jibu maswali Yote katika sehemu hii kwa kutoa maelezo mafupi toshelezi.
3. (a) Eleza kwa ufupi kwa nini mtazamo unaosema kwa dini ni matokeo ya fikra za binadamu katika enzi za ujima si sahihi?
(b) Katika jamii kuna baadhi ya watu wanaodai kuwa hawana dini.Kwa kutumia hoja,kanusha madai ya watu hao.
4. Bainisha njia tano zinazomwezesha mwanadamu kutambua uwepo wa Mola wake katika maisha.
5. Chambua faida nne unazoweza kuzipata kwa kuanza kila jambo jema kwa Bismillahir Rahmanir Rahiim
6. Kutoka kwa Abuu Huraira r.a hakika ya Mtume (S.A.W) amesema: Alama za mnafiki ni tatu, akizungumza husema uongo,akitoa ahadi hatimizi na akiaminiwa hufanya hiyana” [Bukhari na Muslim]
(a) Nini maana ya kuchunga ahadi na kuwa mwaminifu
(b) Je, unakubaliana kwamba uaminifu una faida katika jamii? Eleza kwa ufupi
(c) Bainisha madhara mawili juu ya kuzungumza uwongo katika jamii
7. Wanafunzi wa kidato cha kwanza wameazimia kutekeleza ibada mbalimbali kwa usahihi ili wapate radhi za Allah (S.W). Fafanua mambo matatu yatakayo wawezesha kufahamu vema utekelezaji wa ibada hizo.
8. Fafanua sifa tano (5) za ujumbe wenye kuleta athari chanya katika medani ya Da’awah
9. Historia ya Nabii Ibrahim (A.S) inawafunza waislamu mambo muhimu katika kulingania Uislamu.Bainisha mambo matano tu.
SEHEMU C (Alama 15)
Jibu swali la insha katika sehemu hii
10. Bainisha lengo la khutuba ya ijumaa kasha fafanua mambo manne ya kuzingatia wakati wa kuandaa khutba ya ibada hiyo.
FORM TWO EDK EXAM SERIES 232
FORM TWO EDK EXAM SERIES 232