FORM TWO KISWAHILI NECTA 2025

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA

UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI

021 KISWAHILI

Muda: 2:30 Mwaka: 2025

Maelekezo

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi (10).
  2. Jibu maswali yote kwenye nafasi ulizopewa.
  3. Sehemu A na C zina alama kumi na tano (15) kila moja na sehemu B ina alama sabini (70).
  4. Zingatia maelekezo ya kila sehemu na ya kila swali.
  5. Majibu yote yaandikwe kwa kalamu yenye wino wa bluu au mweusi.
  6. Vifaa vya mawasiliano na vitu visivyoruhiusiwa havitakiwi katika chumba cha upimaji.
  7. Andika Namba yako ya Upimaji katika kila ukurasa sehemu ya juu upande wa kulia.
KWA MATUMIZI YA MPIMAJI TU
NAMBA YA SWALI ALAMA SAHIHI YA MPIMAJI
1.

2.

3.

4.

5.

6.

7.

8.

9.

10.

JUMLA

SAHIHI YA MHAKIKI

SEHEMU A (Alama 15)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1. Katika vipengele (i) - (x), chagua herufi ya jibu sahihi kisha andika herufi ya jibu hilo katika kisanduku ulichopewa.

(i) Mpangilio sahihi wa maneno yafuatayo katika kamusi ni upi?

  1. Shaba, shadidi, shahada, shamba, shangazi
  2. Shaba, shahada, shangazi, shamba, shadidi
  3. Shaba, shangazi, shamba, shadidi, shahada
  4. Shaba, shamba, shangazi, shadidi, shahada
Choose Answer :


(ii) Mwalimu alitufundisha kuwa mizani ni kipengele muhimu cha fani katika ushairi wa fasihi simulizi. Ipi ni maana sahihi ya kipengele hicho?

  1. Silabi au sauti zenye milio ya kufanana katika ubeti
  2. Mstari mzima wa shairi unaojitosheleza kimaana
  3. Mshororo wa mwisho wa kila ubeti wa ushairi
  4. Idadi ya silabi katika mshororo au mstari wa shairi
Choose Answer :


(iii) "Wanafunzi hawapendagi somo la Hisabati kwa kuwa ni gumu." Kosa la kisarufi lililopo katika sentensi hiyo limesababishwa na nini?

  1. Kutozingatia alama za uandishi
  2. Uongezaji wa kiambishi
  3. Udondoshaji wa herufi
  4. Upatanisho wa kisarufi
Choose Answer :


(iv) Sentensi ipi imejengwa na kauli ya kutendewa?

  1. Shamba limelimika lote
  2. Kitabu kimechanika
  3. Mafuta yameisha kabisa
  4. Nyumba imejengewa ua
Choose Answer :


(v) Miundo ya barua ya kindugu na rasmi hutofautishwa na jambo lipi?

  1. Anwani ya mwandishi
  2. Tarehe ya barua
  3. Anwani ya mwandikiwa
  4. Jina la mwandishi
Choose Answer :


(vi) Sentensi ipi si sahihi kuhusu sifa za fasihi simulizi?

  1. Huwasilishwa kwa mdomo
  2. Huwa ni mali ya jamii nzima
  3. Hubadilika kulingana na wakati
  4. Humilikiwa na mwandishi
Choose Answer :


(vii) Sentensi ipi haina kielezi cha mahali?

  1. Anasoma kwa bidii
  2. Anapikia chai jikoni
  3. Anachezea uwanjani
  4. Dereva ameingia barabarani
Choose Answer :


(viii) Nyenzo kuu ya ufahamu wa kusikiliza ni ipi?

  1. Kusoma matini kwa makini
  2. Kutambua aina ya matini
  3. Kusikiliza matini kwa makini
  4. Kujibu maswali kwa makini
Choose Answer :


(ix) Maelezo yapi yanabainisha udhaifu wa kuhifadhi kazi za fasihi simulizi kwa njia ya kichwa?

  1. Haihitaji gharama
  2. Huwasilishwa popote
  3. Humilikiwa na hadhira
  4. Hupotea kwa urahisi
Choose Answer :


(x) Sehemu ya neno inayoundwa na konsonanti na irabu au irabu peke yake na hutamkwa kwa pamoja kama fungu moja la sauti huitwaje?

  1. Sauti
  2. Silabi
  3. Neno
  4. Sentensi
Choose Answer :


2. Oanisha viambishi vilivyopigiwa mstari katika Orodha A na dhima ya kiambishi husika kutoka Orodha B kisha andika jibu sahihi katika kisanduku ulichopewa.

Orodha A Orodha B

(i) Alichokimbia

(ii) Hakuja

(iii) Ninaumwa

(iv) Pigisha

(v) Uliumia

  1. Kiambishi awali cha nafsi ya pili umoja
  2. Kiambishi cha usababishi
  3. Kiambishi awali cha nafsi ya tatu umoja
  4. Kiambishi tamati cha kutendwa
  5. Kiambishi awali cha ukanushi
  6. Kiambishi awali cha urejeshi
  7. Kiambishi awali cha njeo
View Ans


SEHEMU B (Alama 70)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

3. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata:

Wananchi wa Tanzania tunalo jukumu kubwa la kulijenga taifa letu. Tukumbuke kuwa tunapolijenga taifa letu tunawajenga watu wake, kwa kuwa taifa ni jumuiya ya watu. Kuna njia moja muhimu inayoweza kutumika ili kuwafanya watu wajiletee maendeleo yao wenyewe ambayo ni kuelekezwa na kuzingatia maelekezo sahihi ya viongozi wao. Uongozi wa jambo lolote huzingatia kuzungumza na kushauriana na watu, kuwaeleza na kuwashawishi.

Katika nchi ya Tanzania, mazungumzo, ushauri, maelekezo na vishawishi baina ya viongozi na watu katika kuleta maendeleo na kulijenga taifa yanafanyika kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Lugha ya Kiswahili kwa hivi sasa kimekuwa chombo adhimu kinachotuwezesha kupeana maelekezo na kutoa mrejesho wa maelekezo yaliyotolewa.

Kiswahili kimekuwa mstari wa mbele katika kazi kubwa ya kulijenga taifa letu. Ili kazi hii ifanikiwe yatubidi wananchi wote wa Tanzania tujifunze Kiswahili, tukiheshimu na tukitumie katika shughuli zetu zote. Ikiwa tutakibeza na kuamua kwamba kila mmoja wetu ashikilie lugha ya kabila lake, basi yatatukumba matatizo ya ukabila.

Tuangalie nasi tusije tukashindwa kuendelea kujenga nchi yetu kwa sababu ya kukosa maelewano. Kama hatuna lugha ya kutuunganisha tutashindwa kutekeleza majukumu tunayopewa na viongozi wetu, ukiwemo utii wa sheria na kutimiza mipango mbalimbali. Kukosa maendeleo si shabaha yetu, hivyo, jambo kubwa la kwanza yatupasa tufahamu kwamba Kiswahili ndiyo lugha ya taifa tusifanye ajizi tunapaswa kuitumia.

Maswali

(a) Andika kichwa cha habari uliyosoma kwa maneno yasiyozidi matano.

(b) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika habari uliyoisoma:

  1. Adhimu
  2. Tutakibeza
  3. Yatatukumba
  4. Ajizi

(c) Ni njia ipi inashauriwa kutumika katika kuwaletea watu maendeleo?

(d) Fupisha habari uliyosoma kwa maneno yasiyopungua 50 na yasiyozidi 60.

View Ans


4. Kwa kuumia mifano, fafanua tofauti ya msingi iliyopo katika jozi zifuatazo za maneno:

  1. Kivumishi na kiwakilishi
  2. Kitenzi kikuu na kitenzi kisaidizi
  3. Kihisishi na kiunganishi
  4. Nomino dhahania na nomino za pekee
  5. Vielezi vya wakati na vielezi vya mahali
View Ans


5. Eleza dhima moja kwa kila kiambishi kilichopigiwa mstari katika maneno yafuatayo:

  1. Hapigi
  2. Anaondoka
  3. Walikuona
  4. Shikika
  5. Mtu
  6. Viambishi
  7. Hawapo
  8. Watakuja
  9. Huendi
  10. Oana
View Ans


6.Bainisha kosa lililopo katika tungo zifuatazo kisha ziandike tungo hizo kwa usahihi. Kipengele cha (i) kimetumika kama mfano.

(i) Huyu ni lafiki yangu.

Kosa: lafiki

Tungo sahihi: Huyu ni rafiki yangu.

(ii) Rete hicho kitabu.

(iii) Mimi ni mwanainji wa Tanzania.

(iv) Mama anakaaga jikoni anapopika.

(v) Mutu huyu anaumwa.

(vi) Nipe fiatu nivae.

View Ans


7. Eleza kwa kifupi namna njia zifuatazo za mfumo wa mawasiliano zinavyokidhi mawasiliano katika jamii.

  1. Mdomo
  2. Magazeti
  3. Redio
  4. Simu ya mkonomi
  5. Televisheni
View Ans


8. (a) Kamilisha methali zifuatazo:

  1. Kuishi kwingi
  2. hula na wa kwao.
  3. huvikwa pete.
  4. Asiyekubali kushindwa
  5. Jambo usilolijua

(b) Taja njia tano zinazotumika kuhifadhi kazi za fasihi simulizi.

View Ans


9. Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali yanayofuata.

Jembe wangu nakuhitaji, uje unipe neema, Jembe wewe ndiwe chaji, twakuenzi tangu zama, Jembe wewe ni mpaji, wa baba na hata mama, Jembe ndiwe mkombozi, tangu enzi za wahenga.

Jembe wewe wasifika, humtupi mkulima, Jembe shamba tukifyeka, nawe wafanya kulima, Jembe yakija masika, nawe nyuma himahima, Jembe ndiwe mkombozi, tangu enzi za wahenga.

Jembe pengi umefika, ukweli tunausema; Jembe kwetu ukifika, tunapata usalama, Jembe njoo pasi shaka, kisha tujipatie mtama, Jembe ndiwe mkombozi, tangu enzi za wahenga.

Maswali

(a) (i) Shairi hili lina muundo gani?

(ii) Bainisha kituo bahari katika shairi hili.

(b) Eleza dhamira kuu ya shairi hili.

(c) Jembe limepewa uwezo wa binadamu wa kutenda au kufanya jambo. Tamathali gani inayotumika katika fasihi yenye sifa hiyo?

(d) Neno “zama” ni sawa na neno gani katika shairi hili?

(e) Eleza falsafa ya mtunzi wa shairi hili.

View Ans


SEHEMU C (Alama 15)

Jibu swali la kumi (10).

10. Wewe ni mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Chajjaba S.L.P 207, Morogoro na unatarajia kufanya kazi ya kuuza magazeti katika likizo yako ya Desemba mwaka huu. Andika barua kwa Mkurugenzi Mtendaji wa gazeti la Nipashe, S.L.P 1012, Dar es Salaam kuomba kazi hiyo. Jina lako liwe Shukuru Maarifa.

View Ans


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256