FORM TWO HISTORIA MIDTERM EXAMS

Namba Ya Upimaji___________________________

OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA NUSU MUHULA - MACHI 

HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI KIDATO CHA PILI

MUDA : Masaa 2:30

MAELEKEZO

  1. Upimaji huu una sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi (10).
  2. Jibu maswali yote kwenye nafasi ulizopewa.
  3. Sehemu A ina alama kumi na tano (15), sehemu B sabini (70) na sehemu C ina alama kumi na tano (15).
  4. Andika majibu yote kwa kutumia kalamu yenye wino wa bluu au mweusi.
  5. Vifaa vyote vya mawasiliano na vitu vingine visivyonuhusiwa havitakiwi katika chumba cha upimaji.
  6. Andika Namba yako ya Upimaji katika kila ukurasa sehemu ya juu upande wa kulia.

SEHEMU A (Alama 15)

Jibu maswali yote katika sehemu hii

1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika kipengele (i) mpaka cha (x) kisha andika herufi ya jibu sahihi katika sehemu ya karatasi ya mtihani uliyopewa

i. Katika somo la Historia ya Tanzania na Maadili neno Ukoloni lina maana gani?

  1. Hali ya nchi moja kuitawalanchi nyingine katika Nyanja zote za kiuchumi, kisiasa na kiutamadaduni
  2. Hali ya nchikujitawala katika Nyanja zote za kiuchumi, kisiasa na kijamii
  3. Hali ya nchikupigana vita vya ukombozi ili kujinasua na utawala wa kibepari
  4. Hali ya nchi moja kuitawalanchi nyingine katika Nyanja ya kiuchumi na kijamii pekee

ii. Ukoloni ulitokana na kustawi kwa mfumo wa ubepari. Mfumo huu wa ubepariulifikia hatua gani huko Ulayamagharibi hadi kuwalazimuwakolonikuvuka mipaka ya nchi zao ili kutafutarasilimali na masoko mapya za bidhaa zao?

  1. Ujima 
  2. Ubeberu 
  3. Ukabaila 
  4. Ujamaa

iii. Mapinduzi ya viwanda katika nchi za ulayamagharibiyalisababisha ongezeko la mahitaji mbalimbali kama ifuatavyo isipokuwa

  1. Malighafi za kilimo na madini kwaajili ya viwanda
  2. Maeneo ya uwekezaji
  3. Masomo mapya ya bidhaa za viwanda vyao
  4. Matamanio ya kuenezadini ya kiislamu

iv. Mwarabu wa kwanza kutawala kwa pamoja dola za Omani na Zanzibar kuanzia mwaka 1800 hadi 1856 baada ya kufarikialijulikana kama ……

  1. SultaniSeyyid Said bin Sultan 
  2. SultaniSeyyid Majid
  3. Sultani Barghash 
  4. SultaniJamshid bin Abdullah Al Said

v. Ukoloni ulishamiribarani Afrika katika karne za…….

  1. 17 na 18 
  2. 18 na 19 
  3. 19 na 20 
  4. 20 na 21

vi. Katika utawala wa Kijerumani, koloni la Tanganyika lilijulikana kwa jina la…

  1. Afrika mashariki ya Kijerumani 
  2. Tanganyika ya Kijerumani 
  3. Tanzania 
  4. koloni la pwani

vii. Ni mkataba gani wa amani wa mwaka 1919 ulioamuru kwamba makoloni yote yaloyokuwa ya

Wajerumaniyakabidhiwe kwa mataifayaliyoshinda vita kuu ya kwanza ya Dunia?

  1. Mkataba wa amani wa Paris 
  2. mkataba wa amani wa Versailles
  3. mkataba wa amani wa Vienna 
  4. mkataba wa amani wa Laussane

viii. Shughuli za biashara wakati wa utawala wa Waingerezazilifanywa na watu wa jamii ya Kiasia hasa Waarabu na Wahindi pamoja na…….;

  1. A. Makampuni ya kibepari ya Wazungu 
  2. Watafiti wa kizungu
  3. Maafisa wa utawala wa kikoloni 
  4. Jeshi la wakoloni

ix. Mabadiliko ya kisiasa wakati wa utawala wa Waingerezayalihusisha pia kuanzishwa kwa mfumo wa matumizi ya utawala wa kiuwakala. Utawala huu ulianzishwa mwaka 1926 na Gavana wa kiingerezaaliyejulikana kwa jina la.;

  1. Cecil Rhodes 
  2. Carl Peters 
  3. William Mackinnon 
  4. Donald Cameroon

x. Katika utawala wa Waingerezakuliundwashirikisho la machifu, kwa kila kabila kumteuachifummoja kuwa kiongozi mwandamizi wa wengine. ChifuFundikiraaliteuliwa kuongoza machifu wa.?

  1. Kihehe 
  2. Kinyamwezi 
  3. Kisukuma 
  4. Kichaga

MAJIBU:

i
ii
iii
iv
v
vi
vii
viii
ix
x









.

2. Oanisha SAFU A kwa kutoajibu sahihi kutoka katika SAFU B kisha andika herufi ya jibu sahihi katika visanduku chini yake.

SAFU A SAFU B

i. Tanganyikailiwekwa rasmikwenye utawala wa waingereza

ii. walitumiamfumo wa kiuwakala katika utawala wao

iii. Maarufu kwa biasharaya watumwa

iv. Ujerumani ilichukua rasmi mamlaka ya kiutawala Africa ya Mashariki

v. Mwinyi mkuu

  1. 1889
  2. 1919
  3. Waarabu
  4. Wajerumani
  5. Mtawala mwenza wa serikali ya waarabu
  6. Waingereza
  7. Mtawala wa kiarabu

MAJIBU:

i ii iii iv v




.

SEHEMU B (Alama 70)

Jibu maswali yote katika sehemu hii

3. Ukuaji wa mfumo wa ubepari hadi kufikia ubeberu katika robo ya mwisho ya karne ya 19 uliambatana na mapinduzi ya viwanda katika nchi za ulayamagharibi. Kwa hoja tano eleza mahitaji yaliyosababishwa na mapinduzi ya viwanda huko ulaya

4. Wakoloniwalitumia mbinu mbalimbali kuanzisha na kuimarisha tawala zao barani Afrika. Kwa hoja tano eleza mbinu zilizotumika kuanzisha na kuimarisha utawala wa kikoloni katika jamii za Kitanzania.

5. SultaniSeyyidSaid bin Sultan alihamisha makazi yake kutoka Omani kuja Zanzibar mwaka 1840. Kwahoja tano eleza sababu za kiongozi huyo wa utawala wa Waarabukuhamisha makazi yake kuja Zanzibar.

6. Mifumo ya kisiasa na kiuchumi ilikuwa na mchango mkubwa sana katika kukuza maadili ya jamii za asili ya Tanzania, unadhani ni ipi michango ya mifumo hiyo ya kisiasa na kiuchumi katika jamii za asili ya Tanzania.

7. Wakoloniwalijenga njia za uchukuzi na mawasiliano kama vile barabara, reli na bandari. Kwa hoja tano (5) eleza umuhimu wa miundombinu hiyo katika shughuli za serikali za kikoloni

8. Wanafunzi wa shule ya sekondari Kwadoe walitakiwa kufanya utafiti kwa njia ya mtandao ili kubaini tunu mbalimbali za taifa, unadhani ni tunu zipi hizo walizobaini na kuziandika katika ripoti yao.

9. Mabadiliko ya kijamii katika utawala wa Wajerumani na Waingerezayalijikita Zaidi katika utoaji wa huduma za msingi kama elimu, afya, maji, umeme na miundombinu, lengo ni kurahisisha utekelezaji wa malengo ya kikoloni. Kwa hoja tano (5) eleza sifa za elimu ya kikoloni wakati wa utawala wa Wajerumani

SEHEMU C (Alama 15)

Jibu swali namba 10

10. Mchango wa ukoloni katika uhusiano wa Tanzania na mataifayaliyoitawala ni mkubwa sana kwani ulileta mabadiliko mengi katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii katika jamii za kitanzania. kwa hoja sita eleza athari hasizilizotokana na utawala wa kikoloni katika jamii za kitanzania

FORM TWO HISTORIA EXAM SERIES 229  

FORM TWO HISTORIA EXAM SERIES 229  

OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA NUSU MUHULA - MACHI 2026

HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI KIDATO CHA PILI

 MUDA : Masaa 2:30 Machi 2026

MAELEKEZO

  1. Upimaji huu una sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi (10).
  2. Jibu maswali yote kwenye nafasi ulizopewa.
  3. Sehemu A ina alama kumi na tano (15), sehemu B sabini (70) na sehemu C ina alama kumi na tano (15).
  4. Andika majibu yote kwa kutumia kalamu yenye wino wa bluu au mweusi.
  5. Vifaa vyote vya mawasiliano na vitu vingine visivyonuhusiwa havitakiwi katika chumba cha upimaji.
  6. Andika Namba yako ya Upimaji katika kila ukurasa sehemu ya juu upande wa kulia.

SEHEMU A (Alama 15)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1. Kwa kila moja ya vipengee (i)–(x), chagua jibu sahihi kutoka katika mapendekezo yaliyotolewa na andika herufi yake kwenye kisanduku kilichotolewa.

(i) Historia ya Tanzania ni mfululizo wa matukio ya 

  1. kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni na kijamii tangu zamani 
  2. kiuchumi na kisiasa tu baada ya uhuru 
  3. kidini pekee kabla ya ukoloni 
  4. kiuchumi pekee wakati wa ukoloni

(ii) Maadili ya Kitanzania yanatokana na 

  1. mila, desturi, sheria na kanuni za Jamii 
  2. sheria za kigeni pekee 
  3. maadili ya kikoloni tu 
  4. sheria za kidini za kigeni pekee

(iii) Makundi makuu manne ya jamii za Kitanzania ni 

  1. Wabantu, Wanilo, Wakushito na Wakichembe 
  2. Wabantu, Wanyamwezi, Wachagga na Waha 
  3. Wamasai, Wanyakyusa, Wasukuma na Wapare 
  4. Wabantu, Wahehe, Wanyamwezi na Wakara

(iv) Moja ya athari za ukoloni katika maadili ya Kitanzania ni 

  1. kuimarisha umoja wa jamii 
  2. kuanzisha ubinafsi na ushindani badala ya ushirikiano 
  3. kuimarisha umiliki wa pamoja wa ardhi 
  4. kuheshimu viongozi wa jadi zaidi

(v) Ukoloni ulianza kwa nguvu kubwa nchini Tanganyika mwaka 

  1. 1885 (Wajerumani) 
  2. 1890 (Waingereza) 
  3. 1961 (uhuru) 
  4. 1964 (Muungano)

(vi) Sababu kuu ya ukoloni ilikuwa 

  1. kutafuta masoko ya bidhaa za viwanda vya Ulaya 
  2. kuleta elimu kwa Waafrika 
  3. kueneza dini pekee 
  4. kusaidia jamii za Kiafrika

(vii) Moja ya maadili yaliyoharibiwa na ukoloni ni 

  1. umiliki wa pamoja wa ardhi 
  2. ubinafsi na umiliki wa kibinafsi 
  3. ushirikiano wa Jamii 
  4. heshima kwa wazee

(viii) Jamii za Kitanzania zilipinga ukoloni kwa sababu 

  1. walipenda utawala wa kigeni 
  2. walipoteza uhuru, ardhi na maadili yao ya jadi 
  3. walipata faida kubwa kiuchumi 
  4. hawakupendezwa na elimu

(ix) Maadili ya Kitanzania yanachangia 

  1. migogoro na ubaguzi 
  2. mshikamano, amani na tabia njema 
  3. utegemezi wa kigeni 
  4. ubinafsi tu

(x) Ukoloni ulileta mfumo mpya wa maadili unaoitwa 

  1. maadili ya kibepari na ubaguzi wa rangi 
  2. maadili ya umoja na ushirikiano 
  3. maadili ya jadi pekee 
  4. maadili ya kidini tu

2. Oanisha vipengee kutoka ORODHA A na maelezo yanayolingana kutoka ORODHA B. ORODHA A ina vipengee vitano (i-v) vinavyohusu sababu kuu za ukoloni wa Kitanzania, na ORODHA B ina vipengee saba (A-G) vinavyotoa maelezo au mifano yanayohusiana.

ORODHA A

ORODHA B

(i) Kustawi kwa Ubepari na Ubeberu Ulaya Magharibi (Karne ya 19)

(ii) Mahitaji ya Malighafi kwa Viwanda vya Ulaya

(iii) Hitaji la Masoko Mapya na Maeneo ya Uwekezaji Mitaji

(iv) Ushindani wa Kisiasa na Kijeshi kati ya Mataifa ya Ulaya

(v) Kueneza Dini ya Kikristo

  1. Wamisionari kama Ludwig Krapf na Johan Rebman walifika Pwani ya Afrika Mashariki miaka ya 1840 ili kuanzisha vituo vya dini, shule na hospitali, na kupeleka taarifa za kiuchumi kwa serikali zao.
  2. Mataifa kama Uingereza, Ufaransa na Ujerumani yalishindana kwa utukufu wa kitaifa, usalama wa kijeshi na rasilimali zaidi kuliko washindani wao.
  3. Mapinduzi ya Viwanda yaliongeza uzalishaji wa bidhaa, hivyo nchi za Ulaya zilihitaji malighafi na masoko mapya ili kupata faida kubwa.
  4. Viwanda vilihitaji pamba kutoka Tanzania na Uganda, madini kama dhahabu na almasi, mazao kama kahawa na karafuu, pembe za ndovu na mafuta ya mbegu.
  5. Wabepari walitafuta maeneo salama kama Afrika yenye idadi kubwa ya watu na ukosefu wa viwanda vya ndani ili kuuza bidhaa na kuwekeza fedha.
  6. Utawala wa Waarabu ulianza karne ya 18 kwa biashara ya watumwa na karafuu, na sultani Seyyid Said alihamisha makao makuu yake kwenda Zanzibar.
  7. Mkutano wa Berlin wa 1884-1885 uligawanya Afrika bila kumshirikisha Mwafrika, na kuweka mipaka bila kujali jamii au historia.

 SEHEMU B (Alama 40)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

3. Eleza kwa ufupi maana ya maneno yafuatayo: 

  1. Historia ya Tanzania 
  2. Maadili 
  3. Ukoloni 
  4. Jamii 
  5. Utamaduni

4. Toa mifano minne ya makundi ya jamii za Kitanzania na asili zao.

5. Eleza sababu nne kuu za kuanza kwa ukoloni nchini Tanganyika.

6. Eleza athari tano za ukoloni katika maadili ya jamii za Kitanzania.

7. Thibitisha kwa hoja tano kwamba ukoloni ulidhoofisha maadili ya umoja na ushirikiano wa jadi.

8. Eleza umuhimu wa maadili ya Kitanzania katika kujenga taifa lenye mshikamano (hoja tano).

SEHEMU C (Alama 45)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

9. Eleza jinsi ukoloni ulivyoharibu maadili ya umiliki wa pamoja na kuleta umiliki wa kibinafsi (hoja tano).

10. Jadili kwa nini ni muhimu kurudisha na kuimarisha maadili ya jadi ya Kitanzania katika enzi ya kisasa (hoja tano).

11. Toa hoja tano za jinsi historia ya Tanzania na maadili inavyoweza kusaidia katika kuzuia migogoro ya kikabila na kidini leo.

FORM TWO HISTORIA EXAM SERIES 226  

FORM TWO HISTORIA EXAM SERIES 226  

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256